Kando na kuwa ni jukumu la mwanaume kumuapproach na
kumtongoza mwanamke, ni muhimu pia kwa mwanamke kutambua kuwa aliyelala
haamshwi. Usitarajie mwanaume awe na uwezo wa kutambua kuwa umependezwa naye au
la. Ni wajibu wako angalau mara moja au nyingine uhakikishe unatuma ishara fioa
kwa mwanaume ili naye pia awe na interest na wewe.
So utatumia mbinu gani mpaka mwanaume akutambue kuwa uko
interested na yeye? Hizi hapa ni baadhi ya mbinu ambazo ni rahisi za kufanya
ambazo zitamfanya mwanaume aanze ama afikirie kukuapproach mara moja.
#1 Msogelee. Halafu
uvunje vizingiti vya macho kwa kumuangalia machoni kwa muda mrefu halafu kwa
mdomo wake. Hii ni ishara fioa (fiche) ya kumuonyesha kuwa uko wazi kwa yeye
kukupiga busu.
#2 Tafuta nyimbo ya
utambulisho kwako. Cheza nyimbo ambayo itakuwa utambulisho wako na
uhakikishe unafanya mazoezi kwa nyimbo kwayo. Halafu wakati utakapoiskia nyimbo
hio ukiwa out ama katika sehemu flani, utajihisi confidence na poa – na kukupa
ujasiri wa kusalimia yule anayependeza kati ya wote.
#3 Valia vipuli
vikubwa na vya kumeta. Hii inavuta atenshen kwa shingo yako ya upanga – na
pia ni mbinu fioa ya kuonyesha ngozi yako.
#4 Weka ubani ama
ball gum kwa mkoba wako. “Unataka moja?’ ni tamshi rahisi ambalo
litachangia mazungumzo.
#5 Onyesha upande
wako wa furaha. Wakati umeenda sehemu ambayo umemwona mwanaume unayemzimia,
ni bora uonyeshe ule upande wako wa furaha. Cheka na wenzako, furahia nk.
Akikuona tu atakuappoach.
#6 Jifunze stadi ya
kujigongesha mbele ya umpendaye. Wakati umemtambulishaunayemzimia, tembea
ule upande alioko halafu ujigonganishe nayeye kana kwamba hukumuona. “Oh,
samahani. Pole – huwa najisahau mara nyingi ninapozungukwa na wanaume
wakupendeza.” Halafu jitambulishe.
#7 Panga deti ya hapo
kwa hapo. Mtext “Natamani chips na
kebab!! Nataka uache kila kitu sahizi unipeleke katika mkahawa? :)”
#8 Mtese kiasi. Mfano:
Wakati aliyekupendeza anakwambia jina lake ka mara ya kwana, sema, “Wasema?”
ili apate kuegemea karibu yako aweze kujirudia kwa mara nyingine. Halafu sema, “Nini?” huku ukitabasamu.
Utakuwa umeyaanzisha maongezi yenu na ucheshi.
#9 Jifanyie mazoezi
ustadi wako. Ingiza mbinu yako uliyobobea ya kusuka mara moja au nyingine,
kama vile wafanyavyo wahudumu wa kike hotelini. Amini usiamini hili litaongeza
confidence yako wakati unapoongea na mtu unayempenda.
#10 Mwache akuone
unamchungulia. Wakati na wao watakuangalia, tabasamu – itawapatia ile hamu
ya kutaka kukuapproach.
#11 Kuwa interested. Wakati anapoongea na wewe hakikisha kuwa
unaonyesha interest yako kwa kumuuliza maswali ili na yeye apate nafasi ya
kujibu.
#12 Hifadhi mzaha
mmoja. Hii itakuhakikishia kuwa mazungumzo yenu hayatakwama mahali flani.
Na pia iwapo utamfanya acheke basi atakukubali kirahisi.
#13 Mwagize mtoke out
kibahati mbaya. Mtext “Leo usiku una plans gani?” Akikujibu, mwambie,
“Samahani huo ujumbe ulikuwa unaenda kwa rafiki yangu – lakini hakuna shida,
wewe kwaendaje?” Kumwambia hivi kutamfanye afanye ziada.
#14 Angalia nguo
zake. Muulize timu anayoipenda, mchezaji, gemu nk kutokana na mavazi yake.
Bila shaka atagundua kuwa umemnotice.
#15 Jipulize marashi
kwa shingo yako. Hii bila shaka mwanaume unayemzimia atagundua tu.
#16 Tabirika wakati
mwingine. Ule wakati ambao umejigongesha maksudi mbele ya mwanaume,
hakikisha kuomba radhi kwako unakuzidisha kiasi cha kuwa atagundua unajaribu
kufanya maksudi.
#17 Andika jumbe
katika Instagram yake. “Hii picha inachekesha. Hivi ulikuwa unafanya nini
hapa?” Wakijibu sema’ “Unapaswa kuniambia ana kwa ana. :) Wataka hii wikendi
tumeet ama?”
#18 Usimjibu. Jaribu kuitumia hii mbinu. Wakati ambapo
anakutext, usijibu kila swali ambalo atakuwa akikuuliza. Acha maswali mengine
yakielea. Hapa utakuwa unampa wakati wa kukufukuzia zaidi kutaka kukuelewa.
#19 Facebook sinema,
vipindi ama gemu ambazo unataka kuziona. Kama yuko interested na moja wapo ya hizo
basi atapata kisababu cha kutaka mkutane.
#20 Mtambulishe
mvulana anayependeza kwa marafiki zako. Mbinu hii itakupa nafasi kwa
marafiki zako nao kutambulisha wavulana warembo kwako na utakuwa na nafasi ya
kuongea nao.
#21 Pitisha karatasi
iliyoandikwa kwa mkono katika party ambayo inasema, “Nilikuwa nakusalimia!” Ipitishe
kwa mfuko wake - hii inafanya maajabu
zaidi kuliko text za kawaida.
#22 Msuke kabla
hujamuona. Mtext umwaambie, “Unapaswa kuvalia ile tsheti ya blue leo usiku
– inayafanya macho yako yapendeze.”
#23 Mtie
wasiwasi. Hivi ndivyo vya kufanya: Mara ya kwanza
umpendaye anapokutext, mjibu, “Wewe ni nani?” Atakapojieleza,sema, “Lo! ntakosaje
kukutambua?!? :)” Atavutika.
#24 Mpe wakati mgumu.
Wakati ambapo anaonyesha dalili za kukutongoza usikubaliane na yeye hapo
hapo. Msumbue na umpatie wakati mgumu mpaka ile siku utaona imefikia wakati wa
kumkubali.
#25 Mfanye atake
zaidi. Wakati ambao unataka kumuwish gudbye, fanya kumsogelea kana kwamba
unataka kumbusu lakini nenda hadi kwa sikio lake na umwamnie’ “Usiku mwema.”
#26 Mtumie jumbe ya
kumsuku pindi tu atakapokupatia namba yake ya simu. Hii itamshika kwa
saprise. Mfano akikupa namba yake unaweza kumtext neno, “Una tabasamu zuri. Hii
ndio namba yangu.”
#27 Waite. Wakati
umenotice kuwa kuna mtu anakuangalia, mwonyeshe kuwa uko interested naye na
utakuwa na confidence ya hali ya juu. Unaweza kutoa mzaha kama, “Tafadhali
usuniambie kama umeona kitu katikati ya
meno yangu” Hii itamfanya acheke.
#28 Mtumie picha ya
sinema flani. Halafu mwambie “Sinema ya saa kumi – wataka twende? Nitagawa
bisi zangu ikiwezekana.”
Well, hizi ni baadhi ya mbinu ambazo unaweza kutumia iwapo
unataka kumsuka mwanaume yeyote. Usiogope. Aliyelala haamshwi.
Mbinu 30 Rahisi Za Kutongoza Ambazo Unaweza Kutumia Kwa Mwanaume Yeyote
Reviewed by Admin
on
02:05:00
Rating:
