Ushawahi kuwa na rafiki yako, ama una rafiki ambaye tabia
zake sikuhizi zimebadilika? Tabia zake zimekuwa tofauti na kama alivyokuwa
zamani? Rafiki yako huyu umemuona amejeuka ghafla kukupa atenshen yake yote
kwako?
Well, inawezakuwa amependezwa na wewe kiasi cha kuwa
anatamani muwe pamoja. Labda amefall na wewe. Hizi hapa ni baadhi ya mambo
unapaswa kuyaangalia kwa rafiki yako utambue iwapo amekuzimia au la.
#1 Wakati wanapojibu
texts zako wanatumia muda mfupi sana ama muda mrefu kupita kiasi. Kama
anakuchukulia kama rafiki yako wa kawaida basi texts ama jumbe zake huwa
anakutumia kwa mwendo wa kawaida. Lakini kama iwapo ana hisia na wewe utaona
ukimtumia jumbe anakujibu papo hapo, yaani chini ya sekunde moja :) , ama
watapiga hesabu ya kila masaa 5 na dakika 24 ndio wakutumie text nyingine
(yaani kuonyesha kuwa wanapendezwa wakiwa karibu yako)
#2 Wanakutumia text
nyingi zaidi. Hii ni dalili moja
kubwa kwa rafiki yako. Sana sana wao ndio wanaoanzisha maongezi na pia
wanakutumia jumbe kwa wingi.
#3 Kila wakati
wanakuuliza kama unapendezwa na mtu. Mara nyingi maswali haya watakuuliza
wakati usiku wa kiza umewadia na kila kitu kimetulia, nyinyi wawili pekeenu
mkiwa mnachat.
#4 Wanasistiza kuwa hawajapenda mtu kwa sasa. Kwa
kawaida watasema haya yote kwa kuwa tayari washayalenga macho yao kwako
wakiangalia iwapo utawakubali au la.
#5 Hawamkubali yule
unayemzimia ama unayedeti. Ushawahi kuwa katika deti flani halafu rafiki
yako kila wakati anamkashifu unayempenda? Ama kila wakati unapomtajia mwanaume
unayemzimia anakasirika ama atakatiza maongezi yenu? Well, hii ni ishara ya
moja kwa moja kuonyesha kuwa rafiki yako anakupenda wewe.
#6 Wanakualika
muspend wikendi pamoja mkiwa pekeenu. Kama urafiki wenu pamoja na huyu
rafiki yako ulikuwa wa kutangamana na marafiki wengine lakini ghafla wanakualika
muspend Jumamosi nyinyi wawili pekeenu basi hio ni ishara ya moja kwa moja kuwa
kuna kitu kimeanza kupikika. Mukiwa pamoja na marafiki zenu kuna maanisha kuwa
atenshen yote itakuwa kikundini, lakini mukiwa nyinyi wawili itabakia nyinyi
wawili. Ishara ya kuwa anakutaka uwe wake kabisa.
#7 Mara moja anaanza
kukusifia kiundani. Mumezoea kuwa
kila wakati mkiwa pamoja mnaongea kuhusu yule mvulana msiempenda ama habari za
udaku, lakini hii siku moja ameanza kukusifia sifa za kama “Waa! nywele zako
zinanukia utamu.” Halafu hawakwambii jambo hilo tena.
#8 Wanatafuta
visababu vya kukugusa. Wakati ambapo umeangusha neno la kuchekesha,
wanakugusa kwa kukugonga mkono. Wakati ambapo hawajakuona kwa muda wa siku
nyingi anakukumbatia kwa nguvu kiasi cha kuwa unahisi joto lake. Kweli, hapo
kunaweza kuwa na mambo mawili...aidha ni rafiki aliyezoea miguso ama kuna
ajenda ya kuwa amependezwa na wewe.
#9 Watu wanawauliza
iwapo mnadeti. Ama pia wanaweza wasiwaulize sababu wanachikulia nyinyi
wawili mnadeti.
#10 wakati flani
wanaleta mzaha nyote wawili mtoke out pamoja. Wanaweza kusema “Ok, kwa kuwa
leo ni wikendi hatuna kitu cha kufanya. Wewe uko single na mimi niko single, si
tutoke out lakini tuifanye kama deti vile, twende kwa kwa mkahawa halafu twende
sinema tukajienjoy. Kirafiki?”
Hapa moja kwa moja hamaanishi kuwa ni mzaha bali anataka
kujua reaction yako itakuwa vipi. Ukikubali basi atapata nafasi ya kukusogelea
zaidi na zaidi.
#11 Wanataka mpige
picha pamoja. Je hii ni ishara ya kuwa anakupenda? La. Kila siku watu
hupiga picha mara kwa mara. Lakini kama wataanza kuiweka mikono kwa bega ama
kiuno halafu siku ya pili unaiona kwa instagram, ni ishara ya kuwa anakujali –
na labda ni zaidi ya kuwa marafiki.
#12 Wanakufanyia
favour nyingi sana. Kwa mfano anakusindikiza hadi nyumbani kwenu hata kama
mnaishi mtaa wa pili na pia kukulipia bili zako za hotelini. Anakusaidia
kutafuta vitu vyako ulivyosahau pale ulivyoweka na kadhalika...
Well. Hizi ni dalili daharihi kuonyesha kuwa kuna kitu
ambacho rafiki yako anahisi kwako. Je wewe utachukua hatua gani?
Ishara 12 Za Kuonyesha Iwapo Rafiki Yako Amekuzimia
Reviewed by Admin
on
02:02:00
Rating:
