Wanaume ni wengi ambao watakuapproach. Wengine ni wazuri
umependezwa nao na wengine hujapendezwa wao. Lakini je, utajuaje ni mwanaume
yupi anayefaa katika maisha yako? Kuna wanawake wengi ambao wamekabiliwa na
mateso ya kuachwa na mwanaume mmoja hadi mwingine kisa ni kuwa hawajui
kuchagua. Si kila mwanaume anayekuappoach na kukutongoza unapaswa kumkubali.
Kile kinachohitajika kwanza ni kuhakikisha kuwa unamsoma na kuzijua tabia zake
kabla hujaamua kumkubali.
Hapa Dakari Mapenzi tumekuja na vigezo vya kuangalia na
kuchunguza kabla ya kumchagua mwanaume.
Zama nasi...
#1 Huwa anapanga mambo na wewe. Ukimwona mwanaume ambaye anakuhusisha katika
maamuzi yake basi fahamu hapo ndipo. Mwanaume ambaye atakuambia na mapema
kuhusu mambo anayoyapanga wikendi ya kutoka pamoja basi jua huyu ni mwanaume
ambaye anaonyesha dalili za mwanaume bora.
#2 Anakumbuka mambo masuala ambayo uliyazungumza kitambo na
kuyaleta katika mazungumzo yenu. Hapa sio siri. Kila mwanamke anapenda mwanaume
ambaye anakumbuka mambo ambayo alimwambia ama alimfanyia kitambo. Mfano
mwanamke husisimka haswa wakati ambapo mwanaume anamwambia jinsi mara ya kwanza
walipokutana na jinsi alivyovalia. Hii ni ishara dhabiti ya kuonyesha mwanaume
kama huyu anakudhamini. Ukimwona mwanaume ambaye hakumbuki hata jina lako basi
huyo mueke mbali sana.
#3 Haangalii picha zako fb/instagram pekee bali pia ana
comment. Kama unazungumza na yeye kwa comments zako bila tatizo basi huyu hata
mnaweza kuoana naye hapo hapo :)
#4 Kukutumia na kujibu text zako si tatizo. Ukiona mwanaume
anachukua karne nzima kabla kukujibu text yako basi hapo atakuwa labda anawengine
anaowaweka umuhimu zaidi kukuliko. Lakini ukimwona anamakinika na wewe katika
kila jumbe basi hapo ndipo, usichelewe.
#5 Yuko serious na maisha yake ya mbeleni. Mwanaume ambaye
anayapanga maisha yake ya mbeleni ni mwanaume bora kati ya wote. Hii ni ishara
ya kuonyesha kuwa mbeleni hataki kupitia mateso yeyote wakati ambapo atakuwa na
kipenzi chake ubavuni mwake. Hivyo wewe unapaswa kuchukua jukumu la kuhakikisha
kuwa unayafanikisha maisha yake ya usoni kwa kuwa naye.
#6 Hajali iwapo anaonekana mshamba akiwa anadensi. Utafiti
unaonyesha kuwa wanaume ambao hawajui kudensi karibu mara zote huwa ndio
wanakuwa boyfriend bora zaidi.
#7 Anampenda mamake na yule mama mboga. Iwapo mtu anawapenda
wanawake ambao waliyafanikisha maisha yake na pia wale ambao waliyafanya maisha
yake kuwa rahisi, basi pia kwako atakuwa mzuri. Hili ni jambo ambalo
limefanyiwa uchunguzi wa kina.
#8 Anapenda wanyama. Ok ni kusema tu, kuna kitu flani
ambacho kinajitokeza wakati unapomwangalia mwanaume mkubwa akimbabaikia paka mdogo
ambaye analia. “NI LAZIMA UMDETI MWANAUME AINA HII HARAKA SANA.”
#9 Anakufanya ucheke. Kila mwanaume atafanya juu chini
ucheke. Hivyo iwapo unamwona mwanaume anajikakamua ucheke usijilazimishe.
Hakikisha kicheko chako kinatoka naturally kwa mambo ambayo yanakufanya ucheke.
Anyway, ukimwona mwanaume anakupendeza
na vicheko vyake basi ni ishara ya kuwa ni mbora.
#10 Nyote wawili mnazimia kipindi kimoja cha runinga. Hii ni
ishara ya kuwa nyote wawili mko na interest inayofanana, so mkiungana kuwa kitu
kimoja pia si vibaya.
#11 Haongea ubaya kuhusu mpenzi wake wa zamani. Mwanaume
ambaye anatabia za ujentleman basi haitawahi kutokea hata siku moja ambapo
atamtukana ama kumkejeli mpenzi wake wa zamani. Ukiona mwanaume ana tabia kama
hii achana naye mara moja coz pia wewe atakufanyia vivyo hivyo.
#12 Anawaheshimu wanawake. Mwanaume anayewaheshimu wanawake
bila shaka naye atakuheshimu. Hivyo basi usitupe mbao wala kumkataa mwanaume
aina kama hii, ni wachache sana hapa duniani.
Hivi ni baadhi ya mambo ambayo ni dalili ya kuonyesha kuwa
mwanaume flani anafaa kuwa boyfriend wako. Na si lazima aonyeshe ishara hizi zote ndio
umwone anakufaa, la. Iwapo ataonyesha baadhi ya ishara hizi basi usingojee
mpaka apoteze tamaa kutoka kwako.
Mambo 13 Ambayo Humfanya Mwanaume Kuwa Boyfriend Material
Reviewed by Admin
on
02:08:00
Rating: