Ishara Anazoonyesha Kuwa Hatakuwa Boyfriend Wako

Je ishawahi kukutokea? Unakutana na mwanaume ambaye anaonyesha kuwa anapenda kutoka deti na wewe. Mnaspend miezi mitatu mkiwa pamoja, mnatumiana jumbe za sms na kemia ya mapenzi mnaijenga kuwa ya nguvu. Deti ya kwanza inapita kuwa ya tatu, mwezi hadi miezi mitatu inawapita.


Inapita miezi mitatu mkiwa pamoja na huyu mwanaume uliyemzimia, lakini kuna kitu kuhusu mahusiano yenu ambacho kinayafanya mahusiano yenu yasiwe ya shangwe tena. Imepita miezi kadhaa tangu mtoke deti ya kwanza lakini bado hajakufanya wewe kuwa wake. Inafikia pahala flani unaanza kujiuliza iwapo umekuwa ukipoteza muda wako na mwanaume huyu ama bado ni mapema kukata tamaa.

Hili ni jambo la kawaida linalojitokeza kwa wanawake ambao ni single, na ni rahisi sana kuliepuka. Mwanaume ambaye anajitolea kwa mahusiano huwa anaonyesha dalili mwezi wa kwanza wa kudetiana, hivyo lazima uzijue dalili hizi bila kupotezewa wakati wako.

Mwanaume ambaye anajitolea kwa mahusiano utamjua tu, hii ni kwa sababu atafanya juu chini kuhakikisha ya kuwa mahusiano yenu yanakuwa ya shangwe na kuona kuwa una furaha.

Kila siku zinaposonga kwa kudeti na mwanaume, ndipo interest ya kwake inapungua kuwa boyfriend wako kama itapita miezi mitatu bila yeye kuchukua hatua zozote za kuyapanua mahusiano yenu.

So utajuaje kama mwanaume hatakuwa boyfriend wako? 

1. Kama unalala na yeye
Hili si jambo geni. Kulingana na wanaume, wao husema ya kuwa hata kama mwanamke awe mrembo kiasi gani, pindi atakapoanza kulala naye, hupoteza interest kwake. Wazo hili pia limedhibitishwa na wanasayansi kuwa wanaume wanapoteza hamu na mwanamke pindi wanapolala naye.

Hivyo kama mwanamke hufai kutumia nafasi hii ya kumridhisha mwanaume kwa kufanya ngono ukidhania ya kuwa ni silaha yako kuu ya kumnasa. Ngono ni kihamasisho kwa mwanaume na wala si kitu ambacho ni haki yake.

Ni vizuri zaidi kujizuia kutofanya mapenzi na mwanaume hadi ile siku atachukua majukumu yake ya kuendeleza mahusiano yenu mbele. Ukichukua hatua ya kulala na mwanaume mapema utamfanya asijitolee kuendeleza mahusiano yenu.

2. Kama hakuhusishi na mipango yake
Mwanaume ambaye anataka wewe kuwa boyfriend wake atakuhusisha na maisha yake. Lakini kama unajua mipango yake na shughli zake mkiwa naye halafu msipokuwa pamoja hujui mambo yake basi ni dhahiri ya kuwa mwanaume kama huyu hana maslahi yeyote kwako.

Tatizo ni kuwa wanawake wengine hukataa kuamini jambo hili. Ok tuchukulie hivi, wewe kama unampenda mtu fulani ungependa kuwajulisha kitu chochote ambacho unafanya. Hii ni kwa sababu unataka kuwahusisha na maisha yako ili wamakinike sana na wewe.

Vivyo hivyo, mwanaume ambaye amejitolea kuchukua majukumu ya kuendeleza mahusiano yenu  huwa anagawa mikakati na mambo yake kwako. Huwa anafanya hivyo ili kuhakikisha ya kuwa hakutakuwa na mwingine ambaye atakushawishi, atafanya juu chini kuona anafanikiwa kwako.

Hii ni tofauti na mwanaume ambaye atapotea wikendi nzima halafu akupigie simu siku nyingine. Mwanaume kama huyu hayuko serious na mara nyingi ni kuwa aina hii ya wanaume lengo lao ni kukuchezea ama huwa na wanawake wengine wengi.

3. Hakufukuzii
Kuna tofauti kubwa kati ya kukimbiza na kufukuzia. Unaweza kukimbiza kitu ambacho kinakimbia kutoka kwako. Kama mwanaume ameonyesha interest kwako, atakufukuzia kwa njia ambayo atakuonyesha ya kuwa anataka kuwa na mahusiano marefu na wewe. Atakupigia simu mara kwa mara, ataplan jinsi ya kuspend muda mkiwa pamoja na hatokuacha ukibahatisha hisia ambazo anazo kwa moyo wake kukuhusu.

Mwanaume ambaye hajajitolea ni yule ambaye hana mpango wala mikakati yeyote ile. Deti zake anazozipanga zinaonekana kawaida tu na haonyeshi dalili zozote zile za kuwa anakuthamini.


Kumalizia ni kuwa ukiona mwanaume yeyote ambaye ana dalili zozote ambazo tumeziashiria hapa, basi fahamu ya kuwa hakutakii mema. Lakini dalili hizi si kuwa kila mwanaume atamaanisha ya kuwa hajajitolea katika mahusuano bali labda itakuwa hakujua kama majukumu yalikuwa yanahitajika baada ya deti.
Ishara Anazoonyesha Kuwa Hatakuwa Boyfriend Wako Ishara Anazoonyesha Kuwa Hatakuwa Boyfriend Wako Reviewed by Admin on 13:47:00 Rating: 5
Powered by Blogger.