Tabia 12 Tata Ambazo Mwanaume Anapenda Kutoka Kwako

Kuna aina ya wanawake ambao kila mwanamume angependa kuwapeleka nyumbani kwao kukutana na wazazi wake. Hii ni aina ya wanawake ambao tabia zao zinapendeza na za kumfanya awe mwanamke wa ndoa ya milele. Pia kuna ile aina nyingine ya wanawake ambayo kila mwanamume angetamani kuwa nayo. Hii ni aina ya mwanamke ambayo kila mwanamume ndotoni mwake huwa anaifikiria mara kwa mara na angetamani wakati mwingine mpenzi wake kuwa na tabia hizi. Aidha aina hii ya mwanamke hairidhishi kimtazamo wa kijamii kwani inajulikana kuwa 'chafu' kwa kuwa mara nyingi huonekana kama aina ya mwanamke ambayo yeyote akiwa nayo basi milele atakuwa akiteseka kupata maisha ya umakini katika swala la kifamilia.


Tatizo kuu ya mwanamke mwenye tabia chafu ni kuwa anaweza wakati wowote kuiteka hisia ya mwanamume yeyote hivyo basi kama mwanamke haufai kuacha pengo ambalo linaweza kukufanya wewe kupokonywa umpendaye kwa urahisi. Lazima pia kama mwanamke mzuri ujifunze baadhi ya tabia hizi chafu (wanaume tayari wanazipenda) ili iwe kinga kwako kutokana na yeyote yule ambaye anayeweza kuitatiza himaya yako. Hapa tumeweka tabia 12 za mwanamke mchafu ambazo kiloa mwanamume anazipenda.

1. Mwanamke Mtundu
Mwanamke mchafu si yule ambaye anajificha kuonyesha mambo yake anayoyafanya. Hawezi kujifanya kuwa hapendi kuangalia filamu za ngono, ama kuona haya/uoga wa kujaribu mitindo mipya ya kufanya mapenzi. Aina hii ya mwanamke huyafanya maisha ya mapenzi kwa mwanamume yeyote kuwa ya kufurahia na hakuna wakati yatakuwa yanaboa hata mara moja. So lazima ujifundishe jinsi ya kuutumia ujanja huu.

2. Yuko sexy

Vile ambavyo unavaa kuna umuhimu sana kwa mwanamke. Kujifunika maleso nyakati zote ama kufaa nguo nzito nzito si vibaya kwa mwanamke, lakini pia fahamu kuwa kuna nguo ambazo ukizivaa zitamvutia mwanamume. Jaribu kuvaa nguo ambazo zaweza kumfanya mwanamume kuingia na hisia papo hapo.

3. Anapenda kujaribu mambo mapya

Mwanamke mchafu kawaida hajizuii kufanya mambo ambayo hajayaribu kufanya maishani.  Mwanamke kama huyu angependa kujaribu chochote kile hata kama ni mara moja. So kama mwanamke, chukua nafasi kama hii ujitokeze kwa dunia ujaribu mambo ambayo ungependa kuyafanya lakini unaogopa.

4. Wanapenda kusuka
Wanawake wachafu wakati mwingine wanaweza kuwa kama mashetani vile ambao wanaijua sanaa ya kutongoza na kutumia lugha ya ushawishi kwa mwanamume yeyote bila wao kuonyesha azima yao ya kufanya hivyo. Ni wanawake ambao wanafurahisha, wanajua kutumia maujanja na kuzungumza utamu kimapenzi. Wanaweza kumfanya mwanamume yeyote kupandwa na hisia za mapenzi bila hata kuwagusa.

5. Anasimama kujitetea yeye mwenyewe

Mwanamke huyu kwa kawaida anajiamini yeye mwenyewe na kwa kawaida atafanya juu chini kuhakikisha lile ambalo analotaka kutimiza limetimia. Hatazuiwa na yeyote yule. Yeye hatahitaji usaidizi kutoka kwa mwanamume yeyote ili kufanikisha azma yake.

6. Yeye ni yeye

Mwanamke aina hii hahitaji lazima aitikie yale ambayo yanahitajika katika jamii. Si lazima ya yeye kujitweka majukumu ama kufuata masharti na sheria za jamii. Anajua kuwa wengine wanamjua. Lakini ukweli ni kuwa ndani ya mioyo ya watu anaoishi nao, kuna wengine wangetamani kuwa kama yeye ama wengine wangetamani kuwa naye kando yao.

7. Hapaki mafuta kwa mgongo wa chupa
Mwanamke wa kawaida atamshika mwanamume mkono na kumwambia kuwa kila kitu kiko sawa ilhali mambo yanaharibika. Mwanamke mchafu yeye haogopi kukabiliana na ukweli, kama kuna tatizo atamwambia ukweli mwanamume ili tatizo kama hilo walitatue mwishoni.

8. Ni mwanamke ghali kumtunza

Wanaume wangependa kuwa na wanawake ambayo ni rahisi kwao kuwatunza. Lakini wanatamani zaidi kum-maintain mwanamke ambaye ni ghali zaidi akiwa faraghani. Ukweli ni kuwa kila mwanaume ndoto yake ni kuona kuwa ana mwanamke ambaye anatumia hela nyingi kutoka kwake hata kama hana uwezo kama huko.

9. Wanawake wachafu hawajiachilii hivi hivi
Wanawake wengi wa kawaida mara nyingi hujiachilia pindi wanapoingia katika uhusiano mrefu na mwanamume.  Hii inamaanisha kuwa wanaacha tabia za kawaida za kujipodoa na kujirembesha. Baada ya muda utapata kwamba amejiachilia kiasi cha kuwa anaanza kuwa na mafuta mengi mwilini...wanakuwa kama kile kibonzo cha Michelin Tyres. Kwa wanawake wachafu, hii ni kinyume yake kwani hakuna siku atasahau make up wala vipodozi kwani anafahamu mchezo mzima.

10. Wanasema "SITAKI"
Wanaume hawapendi kusikia mwanamke yeyote akichukua misimamo mikali kwao. Lakini baada ya muda flani atachukuliwa kuwa ni mwanamke asiyetaka kuchezewa na wakati wote yeye yuko serious na mambo yake. Mwanamke wa kawaida kwa kuwa hataki kumkosea mwanamume anabakia kukubali chochote kile ambacho ataambiwa na mwishowe kufanywa zuzu ama kuchezewa na mwanamume.

11. Hangojei miujiza itendeke
Yeye ndio hufanya hio miujiza. Hawezi maisha yake yote kungojea yule ambaye atakuja kumtatulia shida ama matatizo yake. Aidha yeye atapambana na dunia kuhakikisha kuwa ametatua matatizo yake, akiwa na usaidizi wa mwanamume yeyote ama yeye mwenyewe.

12. Anajiamini kupindukia
MWanamke huyu anajiamini kupindukia kiasi cha kumfanya mwanamume kuingiwa na woga wa kutaka kumridhisha zaidi. Chochote atakachofanya kuwa anajiamini na kila mtu anamheshimu kwa aina hio ya tabia.

Well, hapo juu ni baadhi ya tabia ambazo zinamfanya mwanamke mchafu kuwapendeza wanaume. Kujiamini na kujifahamu ndio mpango mzima ambao mwanamke huyu anatumia ili kuitawala himaya yake. Hivyo basi kama wewe ni mwanamke wa kawaida unafaa atleast ufanye kuapgrade mchezo wako ili uhakikishe kuwa hujaachwa nyuma.
Tabia 12 Tata Ambazo Mwanaume Anapenda Kutoka Kwako Tabia 12 Tata Ambazo Mwanaume Anapenda Kutoka Kwako Reviewed by Admin on 13:06:00 Rating: 5
Powered by Blogger.